Ishu ya Chama Kutua Yanga; Injinia Hersi Afunguka-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Ishu ya Chama Kutua Yanga; Injinia Hersi Afunguka-Michezoni leo

NI suala la muda tu kwa kiungo Mzambia, Clatous Chama kutua Yanga! Ndivyo wanavyosema Yanga kuhusu tetesi za kumrejesha nchini kiungo huyo wa zamani wa Simba ambaye sasa anakipiga ndani ya kikosi cha RS Berkane kinachoshiriki Ligi Kuu ya Morocco.

 

Chama aliyehudumu kwa mafanikio makubwa ndani ya kikosi cha Simba kwa kipindi cha misimu mitatu, alijiunga na RS Berkane Agosti 16, mwaka huu na kusaini mkataba wa miaka mitatu ambao utamuweka ndani ya klabu hiyo mpaka Juni 30, 2024.

 

Taarifa za Yanga kumuhitaji Chama, zimeendelea kuchukua hatamu ambapo hii siyo mara ya kwanza kutokea kwani kwenye madirisha mawili yaliyopita ya usajili, klabu hiyo ilihusishwa na kiungo huyo.


Makamu Mwenyekiti
wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Injinia Hersi Said, akilizungumzia hilo, alisema: “Chama ni moja kati ya viungo bora kuwahi kucheza katika ligi yetu, tungetamani kuwa naye wakati wowote ule na kwa sasa hakuna kinachoweza kuizuia Yanga kufanya naye mazungumzo.”


Akizungumza na Spoti
Xtra, Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Yanga, Dominic Albinus ‘Baba Paroko’ alisema: “Kwa sasa siwezi nikakanusha wala kukubali kuhusiana na hilo kwa kuwa ni mapema sana kulizungumzia, lakini kama kamati ya ufundi tunafanya kazi kwa karibu na benchi la ufundi, kama kutakuwa na taarifa rasmi basi tutaiweka wazi.”

JOEL THOMAS, DAR ES SALAAM

The post Ishu ya Chama Kutua Yanga; Injinia Hersi Afunguka appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz