GSM Yampa Kiburi Nabi Yanga SC-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

GSM Yampa Kiburi Nabi Yanga SC-Michezoni leo

BAADA ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Azam Jumamosi iliyopita kuichapa Ruvu Shooting juzi bao 3-0, kocha wa Yanga Nasredine Nabi amefunguka kuwa ana ushukuru uongozi wa timu hiyo pamoja na wadhamini wao GSM kwa kufanikisha usajili bora ambao unaendelea kutoa matokeo chanya kila siku.

 

Yanga imefanikiwa kufikisha pointi 12 baada ya kuwachakaza Azam FC na Ruvu katika michezo iliyopigwa klwa nyakati tofauti kwenye Dimba la Mkapa hapa Dar es Salaam.

 

Nabi alisema kuwa anashukuru uongozi mzima wa Yanga na GSM, kwani walimpatia ushirikiano wa kutosha katika kukamilisha usajili wa wachezaji aliokuwa anawahitaji.

 

“ Tunashukuru kwa haya matokeo tuliopata kwani yatatusaidia kuweza kufikia malengo ya timu ya kuchukua ubingwa wa ligi kuu.

 

“Nina ushukuru uongozi mzima wa Yanga pamoja na wadhamini wake GSM kwa sapoti yao kubwa walionipatia katika kipindi cha usajili wamesajili wachezaji ambao nilikuwa nawahitaji pia nina imani kuwa tutafikia malengo yetu kutokana na uwezo mkubwa wa wachezaji wetu,” alisema kocha huyo.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

The post GSM Yampa Kiburi Nabi Yanga SC appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz