Dar yatikisa awamu ya pili Shinda Vitabu vya Shigongo-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Dar yatikisa awamu ya pili Shinda Vitabu vya Shigongo-Michezoni leo

AWAMU ya pili ya Shinda Zawadi ya Kitabu cha Shigongo, imefanyika Novemba 16, 2021 ambapo jumla ya washindi watatu wamepatikana.

Katika awamu hiyo iliyochezeshwa na kuonyeshwa moja kwa moja kupitia Global TV, Dar es Salaam ilifanikiwa kutoa washindi wote watatu ambao ni Irene Elibariki kutoka Tabata, Said Nassoro kutoka Kigamboni na Robert Ndauka wa Temeke.

Kabla ya washindi hao, awali Ismail, Richard Mbano, Philemon Kevin na Khadi Mussa wote wakazi wa Dar es Salaam, Philip Simon Mlimangano kutoka Tabora walikuwa washindi kwenye droo ya kwanza na baadhi wameshapata vitabu vyao.

Magazeti ya Spoti Xtra na Championi, yamekuja na zawadi kabambe kwa wasomaji wake ambapo kupitia magazeti hayo msomaji ataweza kujipatia bure moja ya vitabu vya mwandishi mahiri, Eric Shigongo.

Kwa kununua Gazeti la Spoti Xtra linalouzwa Sh 500 kila siku za Jumanne, Alhamisi na Jumapili, sambamba na Championi linalopatikana Jumatatu, Jumatano, Ijumaa na Jumamosi kwa Sh 800, unapata fursa ya kujishindia moja ya vitabu hivyo.

Miongoni mwa vitabu hivyo ni Rais Anampenda Mke Wangu, Kifo ni Haki Yangu, Machozi na Damu na vingine vya ujasiriamali.

Na Issa Liponda

The post Dar yatikisa awamu ya pili Shinda Vitabu vya Shigongo appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz