Chama Akubali Kurudi Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Chama Akubali Kurudi Simba-Michezoni leo

ALIYEKUWA kiungo wa Simba, Mzambia, Clatous Chama, amebainisha kwamba, yupo tayari kurudi katika kikosi hicho endapo atatakiwa kufanya hivyo.Chama aliyecheza Simba kwa misimu mitatu kuanzia 2018 hadi 2021, msimu huu amejiunga na RS Berkane ya Morocco.

 

Akiwa Simba, kiungo huyo alipata mafanikio makubwa ikiwemo kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2019/20 na kiungo bora 2020/21.

Simba msimu huu imeanza kwa kasi ya kawaida huku kati ya upungufu ambao umekuwa ukibainishwa ni kukosekana kwa Chama na Luis Miquissone ambao waliondoka mwishoni mwa msimu uliopita.

 

Akizungumzia uwezekano wa kurudi Simba, Chama alisema: “Simba ikinihitaji nitarudi kuja kufanya nao kazi maana Simba ni klabu nzuri sana na ninaipenda.

 

“Inaniuma sana kuona Simba inapata matokeo mabaya kwa sasa maana mimi siku zote nawaombea kheri na mafanikio kama wao wanavyo niombea,” alisema Chama na kuongeza:“Kama ningekutana na Simba kwenye michuano ya kimataifa na nikafunga basi ingetegemea, nisingetamani kushangilia.”

Stori: Careen Oscar, Dar es Salaam

The post Chama Akubali Kurudi Simba appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz