Beki Ampigia Magoti Bosi Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Beki Ampigia Magoti Bosi Simba-Michezoni leo

BEKI wa kimataifa wa Simba, raia wa DR Congo, Enock Inonga kabla ya kwenda kuungana na kikosi cha timu yake ya Taifa ya DR Congo, alilazimika kumuomba radhi Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez na viongozi wengine, kufuatia kosa la kadi nyekundu aliyopata dhidi ya Coastal Union.


Inonga kwa sasa yupo kambini na timu
yake ya Taifa ya DR Congo, kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa kufunzu Kombe la Dunia dhidi ya Taifa Stars utakaopigwa kesho Uwanja wa Mkapa jijini Dar.


Chanzo chetu kutoka Simba, kimeliambia
Championi Jumatano kuwa, kabla ya Inonga kuondoka kambini alilazimika kuwaomba upya radhi wachezaji na benchi zima la ufundi lililokuwa sambamba na uongozi wa timu hiyo chini ya CEO wake Barbara, huku akiahidi kutofanya tena kosa kama hilo.


“Wakati Inonga akiaga kwa ajili ya
kujiunga na kikosi chake cha timu ya taifa, alilazimika kuomba radhi kwa mara nyingine kwa wachezaji na benchi la ufundi, huku akiahidi kutoruhusu hasira za aina hiyo kutokea kiasi cha kusababisha kuigharimu timu kwenye mchezo dhidi ya Namungo baada ya kukosekana.

 

“Uongo kwa pamoja na benchi la ufundi ulimsamehe, huku ukimtaka kubadilika kweli na kuwa mfano kwa wenzake na endapo siku nyingine atafanya hivyo basi watalazimika kumfungia na kumkata mshahara kabisa,” kilisema chanzo hicho.

STORI NA MUSA MATEJA | GPL

The post Beki Ampigia Magoti Bosi Simba appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz