Barbara: Wachezaji Wananiomba Waje Kucheza Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Barbara: Wachezaji Wananiomba Waje Kucheza Simba-Michezoni leo

Mtendaji Mkuu wa Simba ‘CEO’ Barbara Gonzalez ameweka wazi kuwa kuelekea katika dirisha dogo la usajili amekuwa akipata usumbufu kutoka kwa mawakala wa wachezaji wakubwa mbalimbali kutoka Afrika wakihitaji wachezaji wao kupata nafasi ya kucheza ndani ya Simba.

 

Simba kwa sasa imekamilisha orodha ya wachezaji 12 wakigeni ambao wanaruhusiwa kusajiliwa kwa mujibu wa kanuni za bodi ya ligi jambo ambalo linawapa ugumu klabu hiyo kuongoza mchezaji wa kigeni mpaka pale itakapoachana na baadhi wa wachezaji.

 

Dirisha dogo la usajili linatarajiwa kufunguliwa Disemba 15 mwaka huu na kufungwa Januari 16 mwakani ambapo timu zitaruhusiwa kufanya usajili kwaajili ya kuboresha vikosi vyao.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu,Barbara alisema kuwa kuelekea katika dirisha dogo la usajili amekuwa akipokea maombi mbalimbali kutoka kwa mawakala wanaomiliki wachezaji wakubwa hapa Afrika wakihitaji nafasi kwaajili ya wachezaji wao kusajiliwa ndani ya Simba ambalo anaamini ni kutokana na ukubwa wa timu na mafanikio ambayo imekuwa ikiyaonyesha.

 

“Nikuambie ukweli tu kuwa nikiwa kama kiongozi wa Simba nimekuwa nikipokea maombi mbalimbali kutoka kwa mawakala wa wachezaji wakubwa barani Afrika wakihitaji nafasi ya wachezaji wao kucheza ndani ya Simba.

 

“Hiyo yote inakuja kutokana na ukubwa wa timu yetu na mafanikio ambayo tumekuwa tukiyapata,kuhusu kama tutafanya usajili katika dirisha dogo kila kitu kitajulikana kutokana na matakwa ya benchi la ufundi hivyo kama kutakuwa na chochote mtafahamu,”alisema kiongozi huyo.

MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

 

The post Barbara: Wachezaji Wananiomba Waje Kucheza Simba appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz