Aucho Augua Ghafla, Aachwa Dar-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Aucho Augua Ghafla, Aachwa Dar-Michezoni leo

YANGA leo watakosa huduma ya kiungo wake fundi Mganda, Khalid Aucho wakati timu hiyo itakapojitupa
uwanjani kuvaana na Namungo
FC.


Timu hizo zinatarajiwa
kujitupa kwenye Uwanja wa Ilulu, Lindi katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kujaaupinzani mkubwa.


Huo ni mchezo wa pili kiungo
huyo mwenye uwezo wa kuchezesha timu na kupiga pasi kuukosa mwingine alioukosa ni ule dhidi ya Ruvu Shooting.


Akizungumza na Championi
Jumamosi, Kocha msaidizi wa timu hiyo, Mrundi Cedric Kaze alisema kuwa kiungo huyo alitua nchini juzi Alhamisi usiku akitokea nyumbani kwao Uganda.


Kaze alisema kuwa mara
baada ya kutua aliomba kubakishwa Dar kwa ajili ya kufanyiwa vipimo kutokana
na kujisikia vibaya na
kuachwa kambini Avic Town, Kigamboni.


“Aucho ana ruhusa ya
viongozi kwa ajili ya kuangalia afya yake ambapo baada ya kuwasili nchini afya yake
haikuwa nzuri akaomba kupata
muda wa matibabu.


“Hivyo hatakuwa sehemu
ya kikosi chetu kitakachocheza dhidi ya Namungo kesho (leo), ataungana na timu baada ya
kurejea Dar,” alisema Kaze

STORI: WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

The post Aucho Augua Ghafla, Aachwa Dar appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz