Yanga Yashtuka, Yawarudisha Azam FC Dar-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Yanga Yashtuka, Yawarudisha Azam FC Dar-Michezoni leo

MABOSI wa Yanga ni kama wameshtukia kitu vile, ni baada ya kuurudisha mchezo wao raundi ya tatu ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja Mkapa jijini Dar es Salaam.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu timu hiyo itangaze mchezo huo kuupeleka Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) hivi karibuni ilitoa nafasi kwa timu kuchagua uwanja wa kucheza michezo ya ligi.

Mmoja wa mabosi wa Yanga, ameliambia Championi Jumatatu kuwa licha ya uwepo wa mashabiki wengi Arusha, uongozi kwa kushirikiana na benchi la ufundi chini ya Mtunisia Nasreddine Nabi wamefikia hatua ya kuubakisha mchezo huo kwa Mkapa.

“Awali tulitangaza mchezo wetu wa ligi dhidi ya Azam kuuepeleka Arusha, hivyo kama uongozi tunafanya kazi kwa kushirikiana na benchi hivyo tumefikia hatua ya kuubakisha mchezo huo hapa Dar.

“Benchi la Ufundi ndiyo lililopendekeza mchezo huo uchezewe hapa Dar, tutakwenda huko katika michezo ijayo ya ligi lakini siyo huu dhidi ya Azam,”alisema bosi huyo.

Alipotafutwa Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela kuzungumzia hilo alisema kuwa “Bado hatujatoa taarifa juu ya hilo, tusubirie kila kitu kitawekwa wazi.”

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

The post Yanga Yashtuka, Yawarudisha Azam FC Dar appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz