Yanga Yapiga Hesabu Kali za Ubingwa-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Yanga Yapiga Hesabu Kali za Ubingwa-Michezoni leo

UONGOZI wa klabu ya Yanga umeweka wazi kuwa mpango wao mkubwa msimu huu ni kuhakikisha wanakusanya pointi tatu muhimu katika kila mchezo ulio mbele yao, ili kuhakikisha wanatangazwa mapema kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara.

 

Mpaka sasa kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu Yanga wamecheza michezo miwili na kuvuna pointi sita ambazo zinawaweka katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, ambapo mchezo wao ujao utakuwa dhidi ya KMC Oktoba 19, mwaka huu katika Uwanja wa Majimaji mkoani Songea.

 

Mara ya mwisho Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ilikuwa msimu wa 2016/17, kabla ya kukabidhi kijiti kwa mabingwa watetezi na watani zao wa jadi Simba, ambao wametwaa taji hilo mara nne mfululizo.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ofisa habari wa klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli alisema: “Kama ambavyo tumeweka wazi kuwa msimu huu malengo yetu makubwa ni kuhakikisha tunatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara, hili siyo la viongozi pekee bali makocha na hata wachezaji wanajua kuhusiana na hilo.”

 

“Ili kufanikisha hilo tumeandaa mkakati wa kuhakikishja tunavuna pointi tatu katika kila mchezo ambao upo mbele yetu, haijalishi tunacheza ugenini au ni katika uwanja gani tunacheza.”

The post Yanga Yapiga Hesabu Kali za Ubingwa appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz