Yanga Waja Kivingine-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Yanga Waja Kivingine-Michezoni leo

UONGOZI wa Yanga umepanga kuja na mikakati mipya itakayowapa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu baada ya kuukosa kwa misimu minne mfululizo.

Msimu huu, Yanga tayari imecheza michezo miwili ya ligi ambayo yote wamefanikiwa kupata ushindi dhidi ya Kagera Sugar na Geita Gold.

Akizungumza na Spoti Xtra, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassani Bumbuli, alisema kuwa moja ya mkakati waliouweka msimu huu ni kuhakikisha wanashinda kila mchezo wa ugenini.

Bumbuli alisema kuwa lengo ni kupata pointi tatu katika kila mchezo, hilo linawezekana kutokana na usajili bora walioufanya msimu huu.

“Tumekuja na mpango mkakati ambao wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wanafahamu, kikubwa ni kufanikisha malengo yetu ya msimu huu.

“Hatutaki kuacha pointi yoyote tunapokuwa ugenini ambako kuna viwanja vibovu. Hatutaki kurudia makosa tuliyoyafanya msimu uliopita. tukipata pointi tatu ugenini basi na nyumbani hatutaki kuacha pointi yoyote,” alisema Bumbuli.

Wilbert Molandi, Dar es Salaam

The post Yanga Waja Kivingine appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz