Yanga SC Weka Mbali na Watoto-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Yanga SC Weka Mbali na Watoto-Michezoni leo

KWA mwendo unaokwenda nao Yanga hivi sasa, unaweza kusema weka mbali na watoto kwani inaziokota tu pointi ndani ya Ligi Kuu Bara na sasa imejikita kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo ikifikisha pointi sita.

 

Hiyo ni baada ya juzi kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Geita Gold katika mchezo wa pili wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar. Katika mchezo huo, bao la Yanga lilifungwa na Jesus Moloko dakika ya 17 akiunganisha pasi ya Yacouba Songne.

 

Awali Yanga iliifunga Kagera Sugar bao 1-0, huku ikiwa imeendeleza mwendo wao mzuri wa kutoruhusu bao katika mechi tatu mfululizo za mashindano ikianza na Ngao ya Jamii ilipoifunga Simba 1-0.

 

Kama washambuliaji wa Yanga juzi wangekuwa makini kutumia nafasi zilizotengenezwa na timu hiyo, pengine wangeibuka na ushindi wa mabao mengi kwani ilishuhudiwa Fiston Mayele na Heritier Makambo kwa nyakati tofauti, wakikosa nafasi za wazi kama ilivyo kwa Moloko na Yacouba.

 

Matokeo ya mechi zingine zilizochezwa Jumamosi ni; Coastal Union 0-0 KMC na Polisi Tanzania 2-1 Azam.

JMUSA MATEJA NA LUNYAMADZO MLYUKA,Dar.

The post Yanga SC Weka Mbali na Watoto appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz