Wenger: Salah Ndiye Bora Duniani-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Wenger: Salah Ndiye Bora Duniani-Michezoni leo

KOCHA wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger amesema kuwa mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah
ndiye bora duniani kwa sasa.

 

Wenger amesema Mmisri huyo amekuwa akifunga mabao ambayo hakuna anayetarajia kuwa anaweza kufunga.
Salah amekuwa moto msimu
huu akiwa amefunga mabao kadhaa muhimu na alifunga mawili kwenye ushindi
wa mabao 3-2 dhidi ya
Atletico Madrid kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, juzi.


Wenger amesema
kuwa mchezaji huyo ni mbunifu, mtengenezaji na mtu ambaye anaweza kufunga mabao kwenye engo yoyote ile.


Salah amekuwa akiweka
rekodi kila mara na juzi aliweka rekodi ya kufunga kwenye michezo tisa mfululizo.
“Salah ni mchezaji mkubwa
sana, nafikiri kwa sasa ndiye mchezaji bora zaidi duniani kwa kuwa naona anaweza kufunga mabao ambayo mchezaji mwingine hawezi kufunga.


“Maisha yake ya nyuma
yanamfanya afanye jambo lolote, aliwahi kucheza soka mtaani na hicho ndiyo kinamfanya aweze kupiga chenga wachezaji watatu wanne kwa pamoja. Ni mjanja na mwenye uwezo mkubwa sana,” alisema Wenger.

The post Wenger: Salah Ndiye Bora Duniani appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz