Uhispania Yaitungua Italia, Yatinga Fainali-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Uhispania Yaitungua Italia, Yatinga Fainali-Michezoni leo

TIMU ya Taifa ya Uhispania imefanikiwa Kutinga Fainali ya michuano ya Uefa Nation League baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Mabingwa wa Ulaya (Euro) Timu ya Taifa ya Italia mchezo uliochezwa usiku wa kuamkia leo Octoba 7, kwenye dimba la San Siro.

 

Mabao ya Uhispania yamewekwa kimiani na mshambuliaji wake Ferran Torres dakika ya 17 na 45 kabla ya kwenda mapumziko huku  nahodha wa mchezo huo beki Leonardo Bonucci akioneshwa kadi nyekundu dakika ya 42 kabla ya Lorenzo Pellegrini kufunga bao dakika 83 la kufutia machozi kwa Italia.

 

Kipigo hicho kimewafanya Uhispania kuvunja rekodi ya Italia ya kucheza michezo 37 mfululizo ya michuano yote bila kufungwa mwaka 2018, rekodi ambayo bado imeshikilia kuwa rekodi ya muda mrefu kwa timu za taifa za wanaume Duniani.

 

Italia imefungwa kwa mara ya kwanza kwenye mchezo rasmi kwenye uwanja wake wa nyumbani tokea mwaka 1999 wakati ambao wachezaji makinda wa Uhispania sita waliokuwa kwenye mchezo wa jana waliokuwa hawajazaliwa ambao ni Pedro Porro, Ferran Torres, Eric Garcia, Bryan Gil, Yeremia Pino na Gavira ‘Gavi’.

 

The post Uhispania Yaitungua Italia, Yatinga Fainali appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz