Tambwe: Kwa Yanga Hii Ningefunga Sana-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Tambwe: Kwa Yanga Hii Ningefunga Sana-Michezoni leo

KINARA wa mabao kwenye ligi ya Championship, Amis Tambwe amesema kuwa kwa Yanga hii ya sasa ilivyokuwa tamu yeye angefunga mabao anavyotaka.

 

Tambwe ambaye alicheza Yanga kwa mafanikio makubwa kwa misimu kadhaa nyuma alisema Yanga ya sasa inacheza vizuri na hata washambuliaji wake wapo bora ila kwake Ingekuwa tofauti kidogo.

 

Akizungumza na Championi, Tambwe alisema: “Yanga wana timu nzuri sana na wanacheza vizuri naamini kama mimi ningekuwepo basi ingekuwa balaa pale mbele kwa sababu kuna kitu cha utofauti nakiona.

 

“Nashukuru Mungu kwa sasa nipo DTB nipo na wenzangu tunapambana kuipandisha timu ligi kuu.”

 

Tambwe amefunga magoli sita kwenye michezo minne ya Championship, huku mchezo mmoja akifunga ‘hat-trick’ na juzi Jumamosi walikuwa na kibarua cha kumenyana na JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Meja Isamuhyo na kumalizika kwa suluhu.

 

“Uwa natazama mechi ya Simba na Yanga kama ambavyo imekuwa desturi ya Watanzania wengi.

ISSA LIPONDA, Dar es Salaam

The post Tambwe: Kwa Yanga Hii Ningefunga Sana appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz