Tambwe Aanza na Rekodi Championship-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Tambwe Aanza na Rekodi Championship-Michezoni leo

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Yanga na Simba, Amissi Tambwe, ameanza na rekodi ya kupiga hat trick kwenye michuano ya Championship msimu huu wa 2021/22 akiwa na kikosi cha DTB.

Tambwe raia wa Burundi, katika mchezo wao wa kwanza msimu huu ndani ya Championship waliocheza jana Jumamosi Uwanja wa Uhuru, Dar dhidi ya African Lyon, alifunga mabao manne wakati timu yake ikishinda 4-1.

Mabao hayo aliyafunga dakika ya 12, 40, 46 na 54, huku lile la African Lyon likifungwa dakika ya 80 kupitia kwa Wilbart Mkimbu.

Matokeo ya mechi zingine zilizochezwa jana ni; Pamba FC 2-1 Kengold, JKT Tanzania 2-1 Mwadui na Ndanda 2-2 Kitayosce.

LEEN ESSAU, Dar

The post Tambwe Aanza na Rekodi Championship appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz