Suti ya Fei Toto Yazua Gumzo – Video-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Suti ya Fei Toto Yazua Gumzo – Video-Michezoni leo

MOJA ya vitu ambavyo vinatesa sana mtandaoni hadi sasa toka tukio la ugawaji wa tuzo za TFF ni mitoko ya mastaa wa Yanga, Dickson Job, Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Shomari Kibwana.

 

Wakati mastaa wengine hasa wa Simba wakipiga mitoko ya maana, wao walichukulia kawaida kama vile wanakwenda sehemu ya kawaida.

 

Wachezaji hao watatu walitinga Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere majira ya saa 3 usiku wakati wale wenzake wakiwepo ukumbini hapo kuanzia saa 12 jioni.

 

Fei Toto ndiye ambaye alikuwa gumzo zaidi, alivalia jinsi ya mtumba pamoja na kiatu cha ngozi, shati la drafti, koti jeusi na miwani. Wakati Job akipiga suti ya mistari, raba na miwani, Kibwana akipiga suruali nyeupe, koti
na shati.

 

Championi Jumamosi lilimtafuta Fei Toto ambaye alionekana kuwa gumzo zaidi ili kujua mtoko huo:
“Kiukweli hatukuwa na makusudi ya
kufanya hivi ilitokea tu, kwa sababu viongozi walitupa taarifa kuwa kuna
ishu ya tuzo.

 

“Ikabidi tuende GSM kutafuta mavazi na kuja hapa, lakini binadamu wamekuwa na fitina sana, wengine wanasema nimeiba koti la Mwakalebela (Fredrick, makamu mwenyekiti wa Yanga) wakati siyo kweli.


“Watu wanaona wivu kwa sababu
tumependeza na aliyeyataka haya yote ni Kibwana, simu yake inapiga picha mbaya sana na ndiyo tumekaa kama walinzi huko mitandaoni.”

The post Suti ya Fei Toto Yazua Gumzo – Video appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz