Staa NBA Aliyegomea Chanjo Asababisha Maandamano-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Staa NBA Aliyegomea Chanjo Asababisha Maandamano-Michezoni leo

Nakuvutia hii kutoka pande za Marekani ambapo maandamano makubwa yamezuka kumsapoti staa wa NBA  Kyrie Irving, anayekiwasha katika timu ya Brooklyn Nets  aliyegomea chanjo ya Corona na kukatazwa kucheza kikapu mpaka akubali kupata chanjo hiyo.

 

Mashabiki wamejazana katika uwanja wa Brooklyn Nets unaoitwa NYC’s Barclays Center kushinikiza staa huyo aruhusiwe kucheza tena kikapu kwani maamuzi ya kuchanjwa ama kutochanjwa ni ya mtu binafsi, video zinazosambaa mitandaoni zinawaonesha mashabiki hao wakiwa kwenye maandamano hayo yaliyoanza tangu jumamosi, zimezua taharuki nchini humo.

Uongozi wa timu ya kikapu ya Brooklyn Nets ulishatoa taarifa mapema mwezi huu kuwa Irving hatoweza kushiriki mashindano ya kikapu mpaka pale atakapokubali kuchoma chanjo ya Corona, nchini Marekani imewekwa sheria ya kila mchezaji kupata chanjo ya Corona hata kama mchezaji haishi katika taifa hilo.

KUMBUKA: Corona (UVIKO-19) ipo na inaua, chanjo inapunguza hatari ya kifo na kupunguza hali mbaya wakati wa kuugua Corona

Cc; @bakarimahundu

The post Staa NBA Aliyegomea Chanjo Asababisha Maandamano appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz