Simba Waitangazia Vita Jwaneng Galaxy ‘Hawatoki’ – Video-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Simba Waitangazia Vita Jwaneng Galaxy ‘Hawatoki’ – Video-Michezoni leo

KLABU ya Simba, leo Oktoba 21, 2021 imezungumza na wanahabari kuelekea mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Jwaneng Galaxy F.C ya Botswana utakaochezwa Jumapili ya Oktoba 24, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar.

Simba wamezindua kauli mbiu yao ‘’It is not over, kazi iendelee’’ kuelekea mchezo wao huo.

Katika mchezo wa ugenini uliopigwa Botswana wiki iliyopita ‘Wekundu wa Msimbazi’ walitanguliza mguu mmoja katika hatua ha makundi baada ya kuibuka na ushindi wa bao 2-0 yaliyofungwa na John Bocco na Tadeo Lwanga.

Viingilio vya mechi ni kama ifatavyo Mzunguka 5,000/- VIP B & C – 20,000/-, VIP A 40,000/ na Platinum 150,000/-

“Maandalizi ya timu yanaendelea vizuri, tayari wachezaji wameingia kambini kujiandaa na mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Wapinzani wetu waliwasili jana.”- Msaidizi wa Afisa Habari, Ally Shatry

 

“Nimeongea na wachezaji wameniahidi kwamba hawatatuangusha. Tununue tiketi kwa wingi na tujitokeze kushingilia chama letu.”- Mhamasishaji wa klabu, Mwijaku.

 

“Tunamwambia mama kwenye soka nchi ipo salama, tumejipanga. Sisi ndio timu pekee ambayo tumeruhusiwa mashabiki 15,000, hilo linaonyesha Simba ni timu kubwa. Twendeni tukashangilie timu yetu.”- Mhamasishaji wa klabu, Kay Mziwanda.

The post Simba Waitangazia Vita Jwaneng Galaxy ‘Hawatoki’ – Video appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz