Sakho, Mugalu Kuwakosa Waswana-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Sakho, Mugalu Kuwakosa Waswana-Michezoni leo

NYOTA wawili wa Simba kiungo mshambuliaji Pape Ousmane Sakho, na mshambuliaji Chris Mugalu wanatarajiwa
kukosekana katika mchezo
wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy, kutokana na
programu ya mapumziko
waliyopewa na timu ya madaktari wa timu hiyo.


Sakho na Mugalu wote
walipata majeraha yao katika mchezo wao uliopita wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Dodoma
Jiji. Simba walishinda 1-0.

 

Nyota hao wawili Jumanne walikosekana katika mazoezi ya Simba yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Boko Veterani kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy
ya Botswana, keshokutwa
Jumapili.


Akizungumza na
Championi Ijumaa, Daktari wa viungo na mchua misuli wa Simba, Fareed Caseem, alisema:
“Tunatarajia kuendelea
kuwakosa wachezaji wetu wawili, ambao ni Pape Ousmane Sakho ambaye alipata majeraha ya kifundo cha mguu na amepewa siku kumi za mapumziko, huku mshambuliaji Chris Mugalu yeye akiwa amepewa wiki tatu za mapumziko.”


Kocha Didier Gomes
ataendelea kukosekana kwenye mechi za kimataifa kutokana na kutokuwa
na vigezo vya Caf huku
Selemani Matola naye akiwa masomoni, hivyo Simba itaongozwa na Mnyarwanda, Thierry Hitimana

The post Sakho, Mugalu Kuwakosa Waswana appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz