Sakho Aandaliwa Kuwaua Wabotswana-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Sakho Aandaliwa Kuwaua Wabotswana-Michezoni leo

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Ousmane Sakho amepata nafuu ya majeraha yake na huenda akawa sehemu ya kikosi hicho kitakachocheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu aanze mazoezi ya timu hiyo yanayoendelea kwenye Uwanja wa Boko Beach Veteran jijini Dar es Salaam.

Kiungo huyo alikuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki moja akiuguza majeraha ya kifundo cha mguu ‘enka’.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Meneja wa timu hiyo, Patrick Rweyemamu alisema kuwa kiungo huyo amemaliza programu ya mazoezi ya binafsi na kesho (leo) huenda akaanza magumu pamoja na timu.

 

Rweyemamu alisema kuwa ataanza mazoezi ya pamoja na timu ili kuhakikisha anakuwa fiti mapema kwa ajili ya mchezo huo wa kimataifa dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

 

“Sakho anaendelea vizuri hivi sasa na huenda akawa sehemu ya kikosi chetu kitakachocheza mchezo wa kimataifa dhidi ya Galaxy.

 

“Kupona kwa Sakho kunafanya kutokuwepo na majeruhi yeyote katika timu baada ya Kanoute (Sadio), kupona kabisa ambaye ameanza mazoezi magumu pamoja na timu tangu wiki iliyopita.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

The post Sakho Aandaliwa Kuwaua Wabotswana appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz