Pique: Hata Tucheze Masaa Matatu Hatufungi Bao-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Pique: Hata Tucheze Masaa Matatu Hatufungi Bao-Michezoni leo

BEKI wa Barcelona, Gerard Pique amesema kuwa timu yao inaweza kucheza kwa masaa matatu uwanjani na bado ikashindwa kufunga bao.

 

Barcelona imekuwa ikionyesha kiwango cha chini sana kwenye Ligi Kuu ya Hispania msimu huu ikiwa imepoteza mchezo wake wa kwanza Jumapili.

 

Timu hiyo imefanikiwa kushinda michezo mitatu tu kati ya saba ambayo wamecheza hadi sasa kwenye Ligi Kuu Hispania msimu huu. Jumapili, Barcelona walilala kwa mabao 2-0 dhidi ya Atletico Madrid mchezo ambao walionyesha kiwango kibovu sana.

 

Pique ambaye alionekana kuzungumza kwa hasira na mchezaji mwenzake Sergio Busquets, amesema hawawezi kufunga bao hata kama watacheza kwa masaa matatu uwanjani. Barca sasa wapo kwenye nafasi ya tisa kwenye wakiwa pointi tano nyuma ya Atletico Madrid ambao wamecheza michezo michache zaidi.

 

“Tulikuwa vizuri na tulionyesha kiwango cha juu sana, lakini ukweli ni kwamba bado tunatatizo kubwa kwenye eneo la ushambuliaji.

 

“Tumefungwa mabao mawili rahisi sana, na kila mmoja anaweza kuona hilo, sina shaka na kila kinachoendelea lakini ukweli ni kwamba tunaweza kucheza hata masaa matatu bila kufunga bao lolote,” alisema Pique ambaye ni mchezaji mkongwe zaidi kwenye timu hiyo.

BARCELONA, Hispania

The post Pique: Hata Tucheze Masaa Matatu Hatufungi Bao appeared first on Global Publishers.





Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??



Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz