Nyoni, Banda Wamtibua Gomes Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Nyoni, Banda Wamtibua Gomes Simba-Michezoni leo

KOCHA Mkuu wa Simba Mfaransa Didier Gomes amesema kuwa ameshindwa kufanya maandalizi mazuri ya mchezo wa hatua ya pili ya Ligi Kuu Bara baada ya wachezaji wake wawili kuchelewa kujiunga na timu hiyo.

 

Hiyo ni katika kuelekea mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliotarajiwa kupigwa juzi dhidi ya Jangwen Galaxy ya nchini Botswana.

 

Wachezaji hao waliochelewa kujiunga na kikosi hicho katika maandalizi ya mchezo huo ni Peter Banda na Duncan Nyoni wote raia wa Malawi.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Gomes alisema kuwa timu hiyo hadi inasafiri kuelekea Botswana hawakufanya mazoezi ya pamoja na timu katika kujiandaa na mchezo huo.

 

Gomes alisema kuwa wachezaji hao wote wameripoti siku moja kabla ya safari ya kuelekea Botswana kutokana na kuchelewa kambini kujiandaa na mchezo huo.

 

Aliongeza kuwa sababu ya kuchelewa kujiunga na timu ni kutokana na kuwepo katika majukumu ya timu yao ya taifa iliyocheza dhidi ya Msumbiji katika mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia.

 

“Siwezi kuwalaumu sana wachezaji wangu Banda na Duncan waliochelewa kujiunga na timu kutokana na kuwepo katika majukumu ya timu yao ya taifa.

 

“Siyo hao pekee pia kukosekana kwa wachezaji waliokuwepo katika majukumu ya timu za taifa wameharibu mipango yangu ya ufundishaji ya kimbinu.

 

“Licha ya kuchelewa kujiunga na timu kambini, nimepanga kuwatumia wachezaji hao katika mchezo dhidi ya Galaxy na mingine,”alisema Gomes.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

The post Nyoni, Banda Wamtibua Gomes Simba appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz