Nabi Awataja Aucho, Bangala Yanga SC-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Nabi Awataja Aucho, Bangala Yanga SC-Michezoni leo

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amefichua kwamba, viwango vinavyooneshwa na mastaa wake wapya, Khalid Aucho na Yannick Bangala, alitarajia kuviona kwani aliamini uwezo wao kabla ya kuwasajili.

 

Nabi alisema kwamba, baada ya kuwafuatilia kwa kipindi kirefu wachezaji hao, ndipo akapendekeza wasajiliwe, hivyo anaamini watafanya makubwa zaidi ndani ya timu hiyo.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha Nabi alisema: “Tumekuwa na mwanzo mzuri wa msimu huu, tayari tumeshinda Ngao ya Jamii, lakini pia tumepata matokeo mazuri katika mchezo wetu wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar.

 

“Kila mtu anajua kuwa hatukuwa na maandalizi bora sana ya kabla ya msimu, lakini tulifanya kazi kubwa katika mchakato wa usajili na mmeona kuna baadhi ya wachezaji wakiwemo Djigui Diara, Aucho na Bangala ambao wameonesha uwezo mzuri, lakini naamini baada ya kuendelea kuwa pamoja watakuwa bora kuliko sasa.”

 

MUKOKO APIGILIA MSUMARI

NAYE Kiungo wa Yanga, Mukoko Tonombe, amesema amevutiwa na uwezo mkubwa wa wachezaji wapya waliosajiliwa ndani ya timu hiyo huku akiweka wazi kuvutiwa zaidi na uwezo waliouonesha Bangala na Aucho.

 

“Timu imefanya usajili mzuri sana, naamini watatusaidia msimu huu, wachezaji wengi wameanza vizuri na nimevutiwa sana na uwezo waliouonesha wachezaji wote wapya ila haswa Bangala na Aucho ambao kimsingi wanacheza katika nafasi ambayo mara nyingi mimi hucheza.

 

“Kuhusu kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha Yanga ni kazi ya mwalimu kujua nani atamtumia, muhimnu zaidi kwangu ni kuona Yanga inapata matokeo mazuri tu na si kingine,” alisema kiungo huyo.

JOEL THOMAS NA MARCO MZUMBE, Dar

The post Nabi Awataja Aucho, Bangala Yanga SC appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz