Nabi Atenga Siku Tisa za Mauaji-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Nabi Atenga Siku Tisa za Mauaji-Michezoni leo

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, amepanga kwamba, baada ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC utakaochezwa Oktoba 19, mwaka huu, atatumia takribani siku tisa kukijenga kikosi chake kuimaliza Azam.

 

Katika maandalizi hayo ya siku tisa kuiwinda Azam, Yanga inatarajiwa kucheza mchezo mmoja wa kirafiki dhidi ya timu kutoka Kenya kati ya Sofapaka au Tusker.

 

Kabla ya hapo, leo Jumapili, Yanga inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya JKU ya Zanzibar kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar.

 

Chanzo kutoka ndani ya Yanga, kimeliambia Spoti Xtra kuwa: “Kocha Nabi hataki masihara kabisa na timu yake kwani baada ya mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, aliomba siku 30 kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake cha msimu huu.

 

“Kwa sasa ndicho anachokifanya kwani kesho (leo) timu itacheza mechi ya kirafiki dhidi ya JKU ya Zanzibar, huku akiwasubiria wale nyota ambao wapo kwenye majukumu ya timu zao za taifa kwa ajili ya kuelekea mkoani Songea kwenye mechi dhidi ya KMC.

 

“Baada ya mchezo dhidi ya KMC timu itaelekea moja kwa moja Arusha ambapo timu itaweka kambi ambayo itakuwa ya takriban siku tisa.

 

“Wakiwa huko watacheza mechi moja ya kirafiki dhidi ya timu ya Kenya kati ya Sofapaka au Tusker ikiwa ni kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC utakaochezwa Oktoba 30, kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.”

LEEN ESSAU, Dar

The post Nabi Atenga Siku Tisa za Mauaji appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz