Nabi Ana Jambo lake Yanga SC-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Nabi Ana Jambo lake Yanga SC-Michezoni leo

KOCHA Mkuu wa Yanga , raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi anachokiangalia hivi sasa katika timu yake
ni matokeo mazuri ya
ushindi pekee na siyo idadi ya mabao, aina ya soka.


Kauli hiyo aliitoa kabla ya
mchezo wao wa Ligi Kuu Bara waliotarajiwa kucheza jana dhidi ya KMC FC
kwenye Uwanja wa Majimaji,
Songea.

 

Yanga imekuwa ikipata matokeo kiduchu katika michezo yake miwili ya ligi ya ushindi wa bao 1-0 waliyoyapata dhidi ya Kagera Sugar nag EITA Gold.


Akizungumza na
Championi Jumatano, Nabi alisema kuwa anachoangalia matokeo mazuri ya ushindi pekee ambayo ndiyo yatakayowawezesha wao kuubeba ubingwa wa ligi.

Nabi alisema kuwa kabla ya ligi kuanza aliomba miezi mitatu ya kuitengeneza timu itakayokuwa imara na itakayoleta ushindani, hivyo muda bado Wanayanga wasubirie muda ufike waone soka safi la kuvutia.


Aliongeza kuwa hivi sasa
anaendelea kutengeneza muunganiko wa timu kwa kuanzia safu ya ulinzi na ushambuliaji ambayo hivi sasa ndiyo inayomuangusha kutokana na kufunga mabao kiduchu.
“Hakuna asiyefahamu
uwezo wa kila mchezaji wangu, kikubwa wachezaji wangu wanahitaji kukaa pamoja kwa ajili ya kutengeneza muunganiko wa timu.


“Hivyo ni lazima nipate
muda mzuri wa kutosha kuiandaa timu itakayocheza soka zuri la kuvutia lile ambalo mashabiki wanalitaka.“Pia kufunga idadi kubwa ya mabao, kwa hivi sasa ninachoangalia ni kuona timu inapata ushindi wa mabao yoyote ikiwemo bao 1-0 kwa lengo la kuongeza idadi ya pointi na siyo kufungwa iwe ndani au nje ya mkoa kwa lengo la kuchukua ubingwa msimu huu,” alisema Nabi.

Stori: Wilbert Molandi, Dar es Salaam

The post Nabi Ana Jambo lake Yanga SC appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz