Nabi Alichonganisha Jembe Jipya na Kibwana Yanga SC-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Nabi Alichonganisha Jembe Jipya na Kibwana Yanga SC-Michezoni leo

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mtunisia, Nasreddine Nabi, amemwambia beki wake mpya David Bryson kuwa ana nafasi ya kucheza mbele ya Shomari Kibwana.

Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni siku chache tangu Bryson arejee uwanjani kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya JKU ya Zanzibar.

Bryson ni kati ya wachezaji wapya waliosajiliwa na Yanga katika msimu huu kwa ajili ya kuiboresha safu ya ulinzi.

Akizungumza na Championi Jumatano, Nabi alisema Kibwana yeye nafasi yake anayotakiwa kuicheza ni beki wa kulia na kushoto alimtumia baada ya mabeki wa kushoto wote watatu Adeyum Saleh, Yassin Mustapha na Bryson kupata majeraha.

Aliongeza kuwa Bryson anatakiwa kupambana ili kujihakikishia nafasi ya kucheza katika kikosi chake cha kwanza licha ya kuwepo Kibwana.

“Bryson ni kati ya mabeki bora ambao wamesajiliwa na Yanga, ana uwezo mkubwa wa kucheza nafasi hiyo. Hivyo ana nafasi ya kucheza licha ya kuwepo Kibwana ambaye yeye ni beki wa kulia.”

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

The post Nabi Alichonganisha Jembe Jipya na Kibwana Yanga SC appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz