Nabi Aanza Kunogewa Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Nabi Aanza Kunogewa Yanga-Michezoni leo

HATIMAYE Kocha Mkuu wa Yanga raia wa Tunisia, Nasreddine Nabi, amefungua kinywa chake na kukiri wazi kwamba, kikosi chake haraka kimeanza kuonesha kupata muunganiko tofauti na alivyotarajia.

 

Yanga ambayo msimu huu ina malengo ya kukusanya mataji ya michuano yote inayoshiriki kwa sasa, imefanya usajili wa wachezaji 11 wakiwemo wazawa na wa kimataifa ambao wana dhamana ya kuipa mafanikio timu hiyo.

 

Malengo yao yameanza kutimia baada ya kubeba Ngao ya Jamii kwa kuifunga Simba bao 1-0.

Chanzo chetu kutoka ndani ya Kambi ya Yanga, yenye makazi yake Avic Town, Kigamboni, Dar es Salaam, kimeliambia Spoti Xtra kwamba, tayari Kocha Nabi ameanza kufurahia muunganiko uliopo kwenye kikosi chake na kubainisha kwamba, suala la kupata ushindi katika mechi zao lina asilimia kubwa.

 

“Kwenye maelezo ya kocha baada ya mchezo wetu na Kagera Sugar, alionekana kuwasifu sana wachezaji wote wakiwemo viungo kama Fei Toto, Khalid Aucho na washambuliaji baada ya kuonekana kuunganika kwa haraka tofauti na matarajio yake.

 

“Pamoja na muunganiko huo, kocha amesema bado kuna dosari kidogo katika eneo la kutoa pasi za mwisho kwani anahitaji mashambulizi ya haraka wanapokaribia ndani ya 18, jambo ambalo kwake anaamini ndani ya mechi tano zijazo atakuwa ameshaanza kupata kile anachohitaji,” kilisema chanzo hicho.

MUSA MATEJA, Dar es Salaam

The post Nabi Aanza Kunogewa Yanga appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz