Mwijaku: Nipo Tayari Kutembea Uchi, Lakini…..!-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mwijaku: Nipo Tayari Kutembea Uchi, Lakini…..!-Michezoni leo

MHAMASISHAJI wa Klabu ya Simba, Mwijaku  amegoma kufanya kile alichoahidi hivi karibuni kwa mashabi wa Simba mbele ya waandishi wa habari, baada ya kutoa kauli yake ya kwamba angetembea utupu bila nguo, endapo Simba ingepoteza katika mchezo wa marudiano wa klabu bingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Mwijaku amedai kwamba alikua tayari kutekeleleza ahadi yake lakini amejua kwamba sheria ya nchi haimruhusu kufanya hivyo.

 

Ikumbukwe klabu ya Simba imeondoshwa katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa msimu huu na Jwaneng Galaxy ya Botswana baada ya kuruhusu kufungwa bao 3-1 nyumbani kwenye mchezo wa juzi jumapili katika dimba la Benjamin Mkapa.

 

Hayo yanajiri baada ya Simba kuruhusu kufungwa mabao matatu nyumbani na kufanya uwiano wa mabao kuwa 3-3 baada ya kushinda 2-0 ugenini hivyo wameondolewa kwa kanuni ya bao la ugenini.

The post Mwijaku: Nipo Tayari Kutembea Uchi, Lakini…..! appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz