MWANARIADHA WA KENYA AKUTWA AMEKUFA NYUMBANI -Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

MWANARIADHA WA KENYA AKUTWA AMEKUFA NYUMBANI -Michezoni leo

Pakua App ya 'EDUSPORTSTZ NEWS' Uweze kufurahia Habari zote za Mapenzi; Udaku, Ajira na Michezo kila siku Ipo Google Playstore, Kwa Ku BONYEZA INSTALL Ili KUIDOWNLOAD Kwenye Simu yako nakutasoma habari zote hata kama hauna MB

MWANARIADHA Agnes Jebet Tirop, aliyeiwakilisha Kenya katika mbio za mita 5000 kwenye Michezo ya Olimpiki ya Tokyo, Japan katika tu ya mwaka huu, amekutwa amefariki dunia jana nyumbani 
huko Iten, Kaunti ya Elgeyo Marakwet.
Polisi nchini Kenya, wanasema Tirop alikutwa amekufa nyumbani kwake kwenye mji wa Iten magharibi mwa Kenya, eneo ambalo hutumiwa na wanariadha wengi kufanya mazoezi.
Aidha, mwili wake umepatikana ukiwa na majeraha tumboni na shingoni na inadaiwa kwamba huenda mumewe ndiye aliyetekeleza kitendo hicho kwa kuwa wamekuwa katika mzozo kwa muda sasa. 
Mumewe Agnes aidha anadaiwa kuonekana nyumbani kwa Agnes saa chache zilizopita kabla ya mwili wake kupatikana.
Taarifa ya shirikisho la riadha nchini kenya imesema "Kenya imepoteza lulu ambae alikuwa kinara anayechipukia katika ngazi za kimataifa, shukrani kwa uwezo wake uwanjani".
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, ametoa ubani kwa mwanariadha huyo kijana na kutoa wito kwa polisi kuwasaka wale waliohusika na mauaji yake.
Ni kitu hakielezeki, hakikupaswa kutokea na ni huzuni kwamba tulepoteza mwanariadha kinda, ambaye katika umri wa miaka 25, ameiletea nchi yake sifa kubwa kupitia jukwaa la kimataifa. Alisema rais Kenyatta katika taarifa yake.
Jumamosi iliyopita, mwanariadha mwingine wa Kenya, Hosea Mwok Macharinyang, mwanamichezo mwingine katika mbio ndefu za kitaifa, alifariki dunia katika kile kimesemwa ni tukio la kujiua.
Macharinyang aliyekuwa na umri wa miaka 35 alikutwa amekufa nyumbani kwake magharibi mwa nchi ya Kenya.
Alikuwa mwanariadha wa kipekee, alijitoa katika mchezo huu na kuishindania Kenya kwa miaka mingi, kuanzia mbio za kitaifa na zile za mita elfu 5 na elfu 10. alisema Jackson Pkemoi, mwakilishi wa shirikisho la riadha kwenye eneo la West Pokot.
Macharinyang aliweka rekodi ya kushindana kwa zaidi ya mara 8, na kushinda mataji matatu mfululizo katika mashindano ya kitaifa kuanzia mwaka 2006 hadi 2008.
Nchi ya Kenya ni miongoni mwa mataifa yenye mafanikio makubwa katika mbio za kimataifa za kitaifa, ikishinda ikiwa na timu 49 na mataji binafsi 27.
Mwezi uliopita mwanariadha huyo alivunja rekodi ya wanawake katika mbio za kilomita 10,000 katika mashindano ya Road to Records Race nchini Ujerumani 
Alishinda pia mashindano ya nyika ya Afrika mnamo 2014 huko Kampala, Uganda na vile vile Mashindano ya Dunia ya nyika kwa Vijana Duniani mnamo 2013 huko Bydgoszcz, Poland.
Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz