Morrison: Nitawavuruga Zaidi Waswana-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Morrison: Nitawavuruga Zaidi Waswana-Michezoni leo

STAA wa Simba, Bernard Morrison amesema kuwa mchezo wao wa kesho Jumapili dhidi ya Jwaneng Galaxy
atacheza kwa juhudi zaidi
ya alivyocheza akiwa Botswana.


Morrison amesema
mchezo huu ndiyo utawapa nafasi wao ya kusonga mbele kwenye hatua ya makundi na kama wakizembea hadithi huenda ikawa tofauti.


Akizungumza na
Championi Jumamosi, Morrison alisema kwenye mchezo wa kwanza alijitahidi kwa kadiri alivyoweza ili kuisaidia timu na ikawa hivyo kwa kupata ushindi na sasa wakiwa nyumbani atawavuruga zaidi Waswana hao.


“Mchezo wa kwanza
ulikuwa mgumu japo tulishinda, naamini wale watakuwa wametusoma sisi
tunachezaje na watakuja
na mpango.

 

Kazi yangu itakuwa moja ambayo ni kucheza kwa juhudi.“Walinichezea hovyo sana nikiwa kwao na nimelijua hilo na sasa itabidi nibadilike mimi pamoja na timu ili tuweze kuwashangaza na kupata ushindi mkubwa zaidi,” alisema Morrison.

Stori: Issa Liponda na Ibrahim Mussa

The post Morrison: Nitawavuruga Zaidi Waswana appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz