Morrison Ampa Kiburi Gomes Simba SC-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Morrison Ampa Kiburi Gomes Simba SC-Michezoni leo

BAADA ya Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes, kukoshwa na viwango vilivyoonyeshwa na mastaa wake wapya akiwengo Duncan Nyoni na kurejea kwa Bernard Morrison ametamba kuwa sasa kilichobaki ni kukusanya pointi tu katika michezo watakayocheza.

 

Simba mpaka sasa katika michezo ya ligi kuu wamekusanya jumla ya pointi nne katika michezo miwili waliyocheza ambapo walitoka sare katika mchezo mmoja dhidi ya Biashara United na kushinda mmoja dhidi ya Dodoma Jiji kwa bao 1-0.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Gomes alisema kuwa amefurahishwa na uwezo waliouonyesha mastaa wake wapya waliosajiliwa ndani ya timu hiyo huku akiweka wazi kuwa kurejea kwa winga Bernard Morrison kutaongeza kitu ndani ya timu hiyo kuelekea katika michezo ijayo kutokana na uzoefu mkubwa wa mchezaji huyo katika ligi kuu.

 

“Nimefurahishwa sana na uwezo waliouonyesha wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu, siwezi kutaja mmoja mmoja lakini wote wameonyesha viwango bora ingawa wamecheza katika viwanja ambavyo siyo rafiki, hii inaonyesha kuwa watasaidia msimu huu kuendelea kufanya vizuri.

 

“Kuhusu kurejea kwa Morrison siwezi kusema sina furaha, hakuna ambaye hafahamu mchango wa Morrison katika michezo yetu.

 

“Ni mchezaji mzuri anayeifahamu ligi hii, hivyo kurejea kwake kutaongeza kitu ndani ya timu kuelekea michezo mingine iliyo mbele yetu ambayo malengo yetu ni kupata matokeo mazuri,” alisema kocha huyo.

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

The post Morrison Ampa Kiburi Gomes Simba SC appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz