Moloko: Yanga ni Zaidi ya AS Vita-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Moloko: Yanga ni Zaidi ya AS Vita-Michezoni leo

WINGA mpya wa Yanga, Jesus Ducapel Moloko, amesema kuwa tangu atue klabuni hapo, amebaini kuwa klabu hiyo ina mashabiki wengi zaidi ya AS Vita ya nchini DR Congo.


Moloko amejiunga na Yanga
katika dirisha kubwa la usajili lililopita ambapo alisajiliwa kuwa mbadala wa winga Tuisila Kisinda ambaye alitimkia RS Berkane ya nchini Morocco.


Winga huyo tangu ajiunge na
Yanga, amekuwa sehemu ya kikosi cha kwanza ambapo tayari amefanikiwa kuifungia timu hiyo bao moja katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Geita Gold ambao Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0.


Akizungumza na Championi
Ijumaa, Moloko alisema kuwa tangu ajiunge na klabu hiyo, amebaini kuwa klabu hiyo ina mashabiki wengi kuliko klabu yake ya awali ya AS Vita ambayo alikuwa akicheza soka kabla ya kuhamia Yanga.


“Yanga ina mashabiki wengi
kuizidi AS Vita, hilo nimeliona angu nimetua ndani ya Yanga, namba ya watu wanaonifuatilia kupitia mitandao ya kijamii ni kubwa sana lakini hata mapokezi ambayo tumekuwa tukiyapata mikoani na hata mashabiki ambao wanahudhuria katika mechi za Yanga ni wengi zaidi ya AS Vita ambapo mashabiki ni wachache wanaohudhuria katika mechi,” alisema winga huyo.

 


“Mtandaoni ndipo
kunaposhangaza kwani nimepata watu wengi sana wanaonifuatilia kupitia Yanga, wakati nikiwa AS Vita wala sikuwa na watu wengi wanaonifuatilia licha ya kucheza katika sehemu kubwa ya timu, baada ya kutua Yanga kila kitu kilibadilika na nilishangaa sana ukubwa nilioupata.”

The post Moloko: Yanga ni Zaidi ya AS Vita appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz