Moloko Aanza Tambo Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Moloko Aanza Tambo Yanga-Michezoni leo

WINGA machachari wa Yanga, Jesus Moloko, anataka kuona akiendelea kufunga mabao katika michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara ili kuhakikisha wanabeba taji hilo.

Hiyo ni siku chache tangu atoke kufunga bao katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Geita Gold kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

Akizungumza na Spoti Xtra, Moloko alisema anataka kuifungia timu yake mabao kwa lengo la kuipa ubingwa wa ligi.

Moloko alisema kuwa anafahamu haitakuwa kazi nyepesi kwake kufunga katika kila mchezo, lakini atajipanga vema kushirikiana na wenzake kufanikisha malengo hayo.

“Binafsi nitafurahi kuona ninaendelea kuifungia timu yangu mabao katika michezo ijayo ya ligi ili kufanikisha malengo ya timu msimu huu.

“Malengo yetu sisi wachezaji, benchi la ufundi na viongozi ni kuchukua ubingwa wa ligi msimu huu.

“Ili hayo yafanikiwe ni lazima kila mchezaji atimize majukumu yake, mimi nimepanga kutimiza majukumu yangu ya kufunga na kutengeneza nafasi za kufungwa kwa wenzangu,” alisema Moloko.

~~WILBERT MOLANDI, Dar

The post Moloko Aanza Tambo Yanga appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz