Mhilu Kuwakosa Wabotswana-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mhilu Kuwakosa Wabotswana-Michezoni leo

IMEBAINIKA kwamba mshambuliaji mpya wa Simba, Yusuph Mhilu, kwa sasa hatashiriki michuano ya kimataifa akiwa na kikosi hicho kutokana na jina lake kuchelewa kuwasilishwa.

 

Mhilu ambaye amejiunga na Simba msimu huu akitokea Kagera Sugar, jina lake lilichelewa kuwasilishwa kutokana na awali usajili wake kuwa na utata.

 

Simba walikuwa na mgogoro na Kagera Sugar ambapo Kagera walikuwa wakihitaji fedha za usajili wa mshambuliaji huyo ambazo hazikuwa zimewasilishwa kwa muda.

 

Katika hatua ya awali, Simba itacheza dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana ambapo mchezo wa kwanza utachezwa Oktoba 17, mwaka huu nchini Botswana, marudiano ni Oktoba 24, Dar.

 

Mtu wa karibu wa mshambuliaji huyo, ameliambia Championi Jumatano kuwa: “Mhilu hataweza kushiriki michuano ya kimataifa ambayo Simba inashiriki kutokana na kibali chake kuchelewa hali iliyosababisha jina lake kuchelewa kutumwa Caf.

 

“Wakati jina lake linatumwa, ilikuwa ni kipindi ambacho muda ulikuwa umeshapita, hivyo hatashiriki kwenye michuano ya kimataifa.

 

“Atabaki kushiriki mashindano ya ndani, labda hapo baadaye ambapo kama Simba watafika mbali, anaweza kuongezwa kwa sababu kuna nafasi ya kufanyika usajili tena.”

Championi lilipomtafuta Mhilu kuzungumzia hilo alisema: “Sipo tayari kuzungumzia ishu hiyo.”

Careen Oscar, Dar es Salaam

The post Mhilu Kuwakosa Wabotswana appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz