Mechi Leo, Biashara United Hawajasafiri Mpaka Sasa-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mechi Leo, Biashara United Hawajasafiri Mpaka Sasa-Michezoni leo

TFF imeliomba Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kusogeza mbele mchezo wa kati ya Al Ahly Tripoli ya Libya dhidi ya Biashara United ya Tanzania hadi Oktoba 27, 2021. TFF imesema licha ya kupatikana ndege ya kukodi safari imeshindikana kwa sababu ya kukosekana vibali vya anga.

 

Biashara United ya Tanzania hadi sasa haijasafiri kwenda Libya kwenye mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Ahly Tripoli, kutokana na changamoto za usafiri wa anga. Mchezo huo umepangwa kuchezwa leo saa 2:00 usiku. Katika mchezo wa kwanza Biashara ilishinda 2-0.

 

Mpaka sasa bado haijatolewa taarifa rasmi iwapo CAF wameridhia maombi hayo ya kusogeza mbele mchezo huo.

The post Mechi Leo, Biashara United Hawajasafiri Mpaka Sasa appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz