Mayele, Makambo Waahidi Mabao Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Mayele, Makambo Waahidi Mabao Yanga-Michezoni leo

BAADA ya kushindwa kufunga bao lolote katika michezo miwili waliyocheza ya ligi kuu mpaka sasa, mastaa wa Yanga, Heritier Makambo na Fiston Mayele wamewatoa wasiwasi mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia watulie kwani mabao yatakuja.

 

Makambo na Mayele wote wameshindwa kufunga mabao katika michezo yao miwili ya mwanzo ya ligi kuu waliyocheza dhidi ya Kagera Sugar na Geita Gold.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Mayele alisema kuwa, ligi ndio kwanza imeanza hivyo kuhusu yeye kufunga mabao bado michezo ipo mingi hivyo bado nafasi za kufunga zipo na atajitahidi kuongeza juhudi ili aweze kufunga mabao katika michezo inayofauta kwani tayari ameshaisoma ligi kuu.

 

“Tayari nimeisoma ligi kuwa inahitaji nini ili niweze kufunga, ligi bado ni changa kuna michezo mingi inayofuata ya ligi kuu ambayo nitajihidi naongeza juhudi na umakini ili niweze kufunga mabao, najua nikiwa kama mshambuliaji nadaiwa mabao na mashabiki wa Yanga hivyo wasiwe na wasi wasi mabao yatakuja,” alisema Mayele.

 

Naye Makambo alisema kuwa: “Kufunga mabao ndio jambo ambalo lipo akilini mwangu, mashabiki wananidai lakini naamini nitatawafurahisha katika michezo mingine, muhimu ni wao kutuombe na sisi kupambana kwa ajili ya timu.”

MARCO MZUMBE, Dar es Salaam

The post Mayele, Makambo Waahidi Mabao Yanga appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz