Man United Yawasiliana na Conte Kumrithi Ole-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Man United Yawasiliana na Conte Kumrithi Ole-Michezoni leo

Klabu ya Manchester United ambayo inatajwa kuwa mbioni kumfukuza kazi kocha wake, Ole Gunner Solskjaer baada ya kipigo cha 5-0 kutoka Liverpool jana, imewasiliana na Kocha Antonio Conte ili kukaa mezani na kuzungumza uwezekano wa kurithi mikoba ya Solskjaer kwa Mashetani hao wekunzu, Sky Sports Italia imethibitisha.

Conte (52) ni mzaliwa wa Lecce Italia na amewahi kufundiaha timu kubwa kama Chelsea 2016-2018 na Inter Milan 2019-2021.

Haya yanajiri baada ya Man United kuchezea kipigo cha bao 5-0 kutoka kwa mahasimu wao, Liverpool usiku wa jana.

Man United wamekuwa na mwendelezo wa matokeo yasiyoridhisha kwa siku za hivi karibuni licha ya uwepo wa nyota wao, Cristiano Ronaldo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu ya Manchester, Richard Arnold amevunja appointment zote za vikao vya wageni ili kukutana na Mmiliki wa Klabu hiyo, Joel Glazer kwa ajili ya kujadili hatima ya Kocha wa Klabu hiyo, Ole Gunnar Solskjaer baada ya kipigo cha jana.

Nini maoni yako? Ole aondoke? Conte aingie?

The post Man United Yawasiliana na Conte Kumrithi Ole appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz