Makambo Atoa Kauli ya Matumaini Yanga SC-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Makambo Atoa Kauli ya Matumaini Yanga SC-Michezoni leo

MSHAMBULIAJI wa Yanga raia wa DR Congo, Heritier Makambo, amewaambia mashabiki wa timu hiyo kwamba, wakimpa muda zaidi, basi watafurahia kuona akifunga mabao mengi kadiri awezavyo.

Makambo ambaye amejiunga na Yanga msimu huu akitokea Horoya AC ya Guinea, aliwahi kuichezea Yanga msimu wa 2018/19 na kuwa kinara wa mabao kikosini hapo ndani ya Ligi Kuu Bara akifunga 17.

Msimu huu akiwa amerudi, bado hajafanikiwa kufunga bao ndani ya Ligi Kuu Bara akicheza mechi mbili, lakini alifunga bao moja wakati Yanga ikifungwa 2-1 na Zanaco kwenye mchezo wa kirafiki katika Wiki ya Mwananchi.

Mtu wa karibu na Makambo, ameliambia Spoti Xtra kwamba: “Makambo kwa sasa akili yake inawaza kufunga tu, hata ukizungumza naye hakuna mahali anajutia kuanzia benchi zaidi anasema yeye ni mfungaji muda wowote anaopewa nafasi na kocha unatosha kabisa kufumania nyavu.

“Kikubwa amewataka mashabiki wote kumvumilia na kumpatia muda na kwamba wasibabaishwe na suala la kuanzia benchi, kwani uwezo wake bado ni mkubwa na siku si nyingi atafungua akaunti ya mabao na kufunga ya kutosha tu.”

MARCO MZUMBE NA HAWA ABOUBAKHARI, DAR ES SALAAM

The post Makambo Atoa Kauli ya Matumaini Yanga SC appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz