Makambo: Subirini Mabao-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Makambo: Subirini Mabao-Michezoni leo

MSHAMBULIAJI kipenzi cha Yanga, Mkongomani, Heritier Makambo, amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia wawe watulivu na wavumilivu wasubirie kuona idadi kubwa ya mabao katika michezo ijayo ya Ligi Kuu Bara.

Hiyo ni salamu kwa mashabiki wa timu hiyo ambao wenyewe wanataka kuona wakipata ushindi wa mabao zaidi ya moja katika michezo yao.

Msimu huu ndani ya Ligi Kuu Bara, Yanga tayari imecheza mechi mbili na kushuhudiwa ikipata ushindi wa 1-0 kwenye mechi zote dhidi ya Kagera Sugar na Geita Gold huku washambuliaji hao wakiwa hawajafunga bao.

Akizungumza na Spoti Xtra, Makambo alisema ni mapema kupewa lawama katika michezo miwili ya ligi waliyoicheza wakati benchi la ufundi likiendelea kutengeneza muunganiko wa timu.

Makambo alisema kuwa kama timu ikitulia, basi mashabiki watarajie kuwaona wakipata ushindi katika michezo ijayo kutokana na ubora wa wachezaji.

“Kwanza kabisa tupongezwe kwa kucheza michezo miwili ya ligi dhidi ya Kagera na Geita Gold bila ya kuruhusu bao.

“Hiyo inamaanisha kuwa muunganiko umeanza kukaa sawa na kama tunatengeneza nafasi nyingi za wazi ambazo tunashindwa kuzitumia katika kufunga, basi ujue tunaanza kuelewana wachezaji.

“Ninaamini kama tukitulia, basi mashabiki wa Yanga watarajie kutuona tukifunga idadi kubwa ya mabao na siyo huo ushindi huo wa bao 1-0 tulioupata katika michezo yetu miwili ya ligi,” alisema Makambo.

r WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

The post Makambo: Subirini Mabao appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz