Magori: Ubingwa Unabaki Kwetu-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Magori: Ubingwa Unabaki Kwetu-Michezoni leo

MJUMBE wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Crescentius Magori, amesema bado malengo ya timu hiyo msimu huu kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara yapo palepale.

 

Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, wameanza ligi hiyo kwa kasi ndogo wakikusanya pointi nne kwenye mechi mbili baada ya kushinda mechi moja na kutoka sare moja.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Magori alisema: “Malengo yetu ni kuhakikisha kuwa tunautetea ubingwa wa ligi kuu msimu huu, tunafahamu kuwa sio rahisi kwa kuwa kuna timu nyingi ambazo zina malengo kama yetu na tumejiandaa kupambana nazo.

 

“Haikuwa rahisi kutwaa ubingwa katika misimu minne mfulululizo, tulipambana haswa kuyafikia mafanikio yale, hivyo hatutokata tamaa.

 

“Tutasimama kwa pamoja kuhakikisha mafanikio ya Simba yanaendelea kuwepo, hivyo msimu huu ubingwa hauendi popote, unabaki kwetu.”

MARCO MZUMBE, Dar es Salaam.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

The post Magori: Ubingwa Unabaki Kwetu appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz