Lusajo Atangaza Kuutaka Ufalme wa Bocco-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Lusajo Atangaza Kuutaka Ufalme wa Bocco-Michezoni leo

KINARA wa chati ya wafungaji bora kwenye Ligi Kuu Bara mpaka sasa, Reliants Lusajo amefunguka kuwa malengo yake makubwa ni kuhakikisha anafunga mabao mengi zaidi msimu huu ili kutimiza ndoto yake ya kutwaa kiatu cha ufungaji bora ambacho kinatetewa na nahodha wa Simba John Bocco.

 

Lusajo katika michezo miwili iliyopita ya Namungo amefanikiwa kufunga mabao mawili, akifunga bao moja kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar na mchezo dhidi ya Geita Gold. Mshambuliaji huyo msimu wa 2019/20, akiwa na kikosi cha Namungo alifanikiwa kuibuka mfungaji bora namba nne naada ya kufunga mabao 12.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Lusajo alisema: “Kama kikosi tumekuwa na mwanzo mzuri wa msimu huu ambapo mpaka sasa hatujapoteza mchezo wowote katika michezo yetu miwili ya kwanza, lakini nafurahi pia kuanza vizuri kwa kufunga mabao mawili katika michezo hiyo.

 

“Malengo ya kila mshambuliaji ni kuhakikisha anafunga mabao, hivyo natumaini nitaendelea kuwa katika kiwango bora kama ilivyo sasa, na kufunga mabao mengi ili kutimiza malengo yangu ya kushinda tuzo ya mfungaji bora.”

JOEL THOMAS, Dar es Salaam

The post Lusajo Atangaza Kuutaka Ufalme wa Bocco appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz