Kipa Mpya Yanga SC Azidiwa Uwezo na Kabwili-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Kipa Mpya Yanga SC Azidiwa Uwezo na Kabwili-Michezoni leo

KOCHA wa Makipa Yanga, Razack Siwa amefunguka kuwa kinachomzuia kipa wake, Erick Johora kucheza tangu kuanza kwa msimu huu ni ushindani mkubwa anaopata kutoka kwa makipa wenzake ambao ni Djigui Diarra na Ramadhan Kabwili.

 

Johora tangu asajiliwe Yanga kwenye dirisha kubwa la usajili hajawahi kucheza mchezo wowote wa ligi pamoja na ile ya Ligi ya Mabingwa pia ule wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Siwa alisema kuwa: “Nafikiri wote ni makipa wazuri sana kusema ukweli ila nadhani ni changamoto na ushindani mkubwa uliopo ndio maana kila mmoja anataka kupambana ili atimize malengo yake.

 

“Nafasi ya kipa ni moja tu uwanjani tofauti na maeneo mengine kama mabeki, viungo na hata washambuliaji kwa hiyo unapopata nafasi unatakiwa upambane sana na uitendee vema ili anapokuja mwingine aweze kupambana zaidi yako.

 

“Johora hajapata nafasi tu kwenye kikosi ila ni kipa mzuri sana nina imani akipata nafasi anaweza kuonyesha kitu na akapata nafasi kwenye timu kama hao wengine wanavyopata nafasi,“ alisema Siwa.

Leen Essau, Dar es Salaam

The post Kipa Mpya Yanga SC Azidiwa Uwezo na Kabwili appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz