Kichapo cha Fury Chamchafua Wilder-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Kichapo cha Fury Chamchafua Wilder-Michezoni leo

KOCHA wa Bondia Deontay Wilder anayeitwa Malik Scott ametoa Taarifa za Bondia wake kuhusu majeraha aliyoyapata kwenye mchezo dhidi ya Tyson Fury, uliounguruma Jumamosi (Oktoba 09).

 

Scott amesema bondia wake amepasuka mdomo wa chini, ngoma ya sikio, amevunjika kidole kimoja cha mkono wa kushoto pamoja na kuvunjika Knuckles katika maunganiko ya videlo na mkono wa kulia.

 

“Nimejiskia vibaya sana kwa Wilder kupata majeraha yote hayo ila ndiyo pesa inavyotafutwa,” amesema Scott.

 

Hata hivyo taarifa njema ni kuwa, mkataba waliosainia kati ya Tyson Fury na Deontay Wilder walikubaliana kila mmoja kuingiza kiasi cha Dola za kimarekani Milion Tano sambamba na malipo ya haki za Televisheni ambayo ni zaidi ya Dola Milion 20.

 

Kutokana na mgawanyo huo wa fedha, Tyson Fury amepata Dola Milion 30 na Deontay Wilder amepata Dola Milion 20 kutoka kwenye malipo ya haki za Televisheni.

The post Kichapo cha Fury Chamchafua Wilder appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz