Kaze Atangaza Hali ya Hatari Yanga-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Kaze Atangaza Hali ya Hatari Yanga-Michezoni leo

KOCHA Msaidizi wa Yanga, Mrundi, Cedric Kaze, amesema siku 15 za kambi ya mkoani Arusha watazitumia kutengeneza muunganiko katika safu yao ya ushambuliaji.

Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni siku chache tangu timu hiyo itoke kucheza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Geita Gold uliochezwa wiki iliyopita na Yanga kushinda 1-0, mfungaji akiwa Jesus Moloko.

Timu hiyo inatarajiwa kusafiri kuelekea Arusha kwa ajili ya kambi fupi kupisha michezo ya timu ya timu za taifa.

Akizingumza na Spoti Xtra, Kaze alisema anaamini watakaporejea katika ligi watakuwa imara zaidi na kuendelea na kasi yao ya ushindi.

Kaze alisema kuwa, wamepanga kutumia siku 15 kwa ajili ya kambi mkoani huko, kikubwa wataziboresha sehemu zote zenye upungufu ili kuhakikisha wanafikia malengo waliyojiweka ya kupata ushindi katika kila mchezo.

Aliongeza kuwa sehemu watakayoanza nayo kuifanyia kazi ni ushambuliaji ambayo inashindwa kutumia nafasi nyingi za kufunga mabao ambayo inaongozwa na Fiston Mayele, Heritier Makambo na Yusuph Athumani.

“Mechi mbili tumepata ushindi na kukusanya pointi sita, licha ya kuendelea kuimarika katika baadhi ya nafasi katika timu yetu ya Yanga, lakini tatizo lililopo ni kwenye ushambuliaji ambapo benchi la ufundi tumepanga kulifanyia kazi kwa siku 15 tutakazokaa Arusha.

“Kikubwa mashabiki waendelee kutusapoti ili kuhakikisha tunafanikisha malengo yetu ya msimu ya kubeba ubingwa wa ligi,” alisema Kaze.

~~WILBERT MOLANDI, DAR

The post Kaze Atangaza Hali ya Hatari Yanga appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz