Kapombe Ashusha Presha Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Kapombe Ashusha Presha Simba-Michezoni leo

BEKI mkongwe wa kulia wa Simba, Shomari Kapombe, ameshusha presha katika timu hiyo baada ya kupata nafuu ya majeraha yake ya kifundo cha mguu ‘enka’.

 

Kapombe alipata majeraha hayo katika mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United uliochezwa Mara. Katika mchezo huo, Kapombe alishindwa kumaliza dakika zote na kutolewa, huku nafasi yake ikichukuliwa na Mohammed Hussein ‘Tshabalala’.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Daktari Mkuu wa Simba, Yassin Gembe alisema beki huyo anaendelea vizuri baada ya kupata nafuu na huenda akawepo katika mchezo ujao dhidi ya Polisi Tanzania.

 

Gembe alisema kuwa beki huyo alipata majeraha madogo katika mchezo huo, lakini kwa hofu ya kupata maumivu zaidi wakampumzisha kwa makusudi.

 

“Kapombe amepata nafuu ya majeraha yake ya enka, ameanza mazoezi mepesi ya binafsi hivyo atakuwepo katika mchezo dhidi ya Polisi Tanzania.

 

“Kupona kwake kutaimarisha kikosi kutokana na umuhimu mkubwa wa Kapombe katika kikosi chetu,” alisema Gembe.

WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

 

The post Kapombe Ashusha Presha Simba appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz