Kanoute Akabidhiwa Wabotswana-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Kanoute Akabidhiwa Wabotswana-Michezoni leo

KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes, ana matumaini makubwa ya kumtumia kiungo wake, Sadio Kanoute raia wa Mali kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mchezo wa hatua ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy kutokea Botswana.

 

Oktoba 17, mwaka huu, Simba itapambana na timu hiyo, kisha kurudiana Oktoba 22, ambapo mshindi wa jumla anaenda hatua ya makundi huku atakayepoteza akicheza mechi za mtoano dhidi ya walioshinda mechi za Kombe la Shirikisho Afrika kutafuta nafasi ya kutinga makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Gomes alisema: “Kama mnavyojua tulimkosa Kanoute katika michezo miwili iliyopita ya Ligi Kuu Bara kutokana na majeraha, lakini tunashukuru kwa sasa amepona kwa asilimia kubwa.

 

“Tunamuhitaji katika mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Galaxy ili kupata matokeo chanya, kwa kuwa ni mchezaji muhimu kwetu ambaye tayari ameonesha wazi kwa kila mtu kuwa ni miongoni mwa viungo bora kwa sasa kutokana na uwezo mkubwa alionao.”

JOEL THOMAS, Dar

The post Kanoute Akabidhiwa Wabotswana appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz