Gomes: Ubora wa Wabotswana Upo Hapa-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Gomes: Ubora wa Wabotswana Upo Hapa-Michezoni leo

KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes, amewatazama wapinzani wake Klabu ya Jwaneng Galaxy ya nchini Botswana huku akiweka wazi ubora wao katika safu ya kiungo na ushambuliaji.

Simba itaifuata Jwaneng Galaxy kule Botswana katika mchezo wa kwanza wa hatua ya kwanza ya mtoano utakaochezwa Oktoba 17, huku mchezo wa marudiano ukitarajiwa kuchezwa Oktoba 24 katika Uwanja wa Mkapa, Dar.

Akizungumza na Championi Jumatano, Gomes alisema: “Tayari nimewatazama wapinzani wetu Jwaneng kutoka Botswana, ni timu nzuri yenye ubora mkubwa hasa katika eneo la kiungo na eneo la ushambuliaji, tunahitaji kuwa bora zaidi yao ili tuweze kupata matokeo mazuri.

“Tuna maandalizi mazuri mpaka sasa, tumecheza michezo miwili ya kirafiki ambayo imetusaidia kuzidi kuwa imara kabla ya kusafiri kwenda katika mchezo wetu, tunahitaji kupambana haswa ili kupata kile tunachohitaji,” alisema kocha huyo.

Marco Mzumbe, Dar es Salaam

The post Gomes: Ubora wa Wabotswana Upo Hapa appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz