Gomes Awashtukia Wabotswana-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Gomes Awashtukia Wabotswana-Michezoni leo

KUONDOKA kwa baadhi ya mastaa wa Simba ambao wamejiunga na timu zao za Taifa, kumemfanya kocha mkuu wa timu hiyo, Didier Gomes, kusitisha mazoezi ya kimbinu mpaka pale wachezaji wote watakaporejea.

 

Simba imetoa wachezaji 15 kutoka mataifa sita ya Afrika ambao wameitwa katika timu zao za taifa. Baada ya kumalizika kwa ratiba ya mechi za kimataifa, Oktoba 17, mwaka huu, Simba itakuwa ugenini kucheza dhidi ya Jwaneng Galaxy, mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Kocha wa Viungo wa Simba, Adel Zrane, alisema: “Wachezaji ambao hawajaitwa kwenye vikosi vya timu zao za taifa wanaendelea vizuri na mazoezi kwa ajili ya kujiweka sawa kujiandaa na ratiba ya michezo iliyo mbele yetu.

 

“Lakini mazoezi yetu kwa sasa ni yale yaliyojikita katika kuimarisha utimamu wa mwili, kuhusiana na mazoezi ya kimbinu kocha mkuu Gomes ameweka wazi kuwa lazima tuwe na kikosi kamili.

 

“Hivyo kuhusiana na mazoezi ya kimbinu tunasubiri mpaka wachezaji wetu wote waliopo na timu za taifa warejee.”

 

Gomes ameona kuwapa mbinu nyota wachache itakuwa ni sawa na kazi bure, hivyo anawasubiri wajumuike wote ili kuwaandalia dozi Wabotswana ambapo malengo ni kufika mbali katika michuano hiyo msimu huu.

JOEL THOMAS, Dar es Salaam

The post Gomes Awashtukia Wabotswana appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz