Gomes atamba na Kagere Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Gomes atamba na Kagere Simba-Michezoni leo

KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes kwa mara nyingine tena ameibuka na kutoa kauli ya kibabe kumpandisha straika wake hatari raia wa Rwanda, Meddie Kagere, kutoka nyota mbili hadi tano kwa kuahidi kumtumia mechi nyingi za Ligi Kuu Bara.

 

Kagere ameitwa kwenye timu yake ya taifa ya Rwanda, itakayokutana na Uganda, katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu Bara, Kagere aliipatia pointi tatu, Simba baada ya kuwanyuka Dodoma Jiji bao 1-0, akitokea benchi.

 

Akizungumza mbele ya Championi Jumatano, Gomes aliweka wazi kwamba tayari ameisoma Ligi Kuu Bara, msimu huu wa 2021/22, hivyo kufuatia namna ya uchezaji wa timu pinzani ameahidi kuhakikisha anatumia washambuliaji wenye nguvu kama ilivyo kwa Kagere ili kuendana na hali.

 

“Kwa mechi zetu zijazo ni wachezaji wale wenye nguvu nyingi na akili nitawatumia kwa sababu tulifanya makosa kwenye mechi zetu za mwanzo kabla ya kujua namna ligi inavyokwenda hasa kwa kuwa ni mwanzo tulishindwa kujua mambo yatakuaje. wachezaji wenye nguvu na akili hao nitawatumia.

 

“Mchezo wetu ujao ni dhidi ya Polisi Tanzania na utakuwa ni kwenye ligi, nawatambua vizuri wapinzani wetu najua ni timu nzuri kwa kuwa inafanya vizuri. Haina mashaka kwa upande wetu kwa kuwa nasi tuna wachezaji wazuri na wanahitaji kupata matokeo hivyo ni suala la kusubiri na kuona itakuaje,” alisema Gomes.

Musa Mateja, Dar es Salaam

The post Gomes atamba na Kagere Simba appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz