Gomes Ataja Dakika za Mabao Simba-Michezoni leo - EDUSPORTSTZ

Latest


 

Gomes Ataja Dakika za Mabao Simba-Michezoni leo

KOCHA Mkuu wa Klabu ya Simba, Didier Gomes amefunguka kuwa amebaini timu nyingi za ligi kuu huwa zinabadilika kiuchezaji zinapocheza dhidi yao na wachezaji huwa wanakamia sana.

 

Gomes alisema kwa sababu hiyo ameona jambo pekee ambalo wanatakiwa kwenda nalo ni kupata matokeo mapema ili kupunguza presha kwa wachezaji wakati mchezo ukiwa unaendelea.

 

Gomes alisema sababu kubwa ya wachezaji wake kufanyiwa madhambi mara kwa mara ni kutokana na wapinzani wao kucheza kwa kukamia na kulazimisha kupata matokeo mbele ya Simba.

 

“Tumecheza mechi mbili za ligi na tumefanikiwa kuona nini tunatakiwa kufanya kwenye kila mchezo. Timu nyingi zikiwa zinacheza dhidi yetu huwa zinabadilika na kucheza kwa nguvu sana.

 

“Siyo jambo baya kwa sababu kila timu inahitaji matokeo, kwa upande wetu tumekaa chini na kujua nini tunatakiwa tufanye ili kuepukana na presha ndani ya uwanja, lazima dakika za mwanzo tuwe tumepata mabao,” alisema Gomes.

ISSA LIPONDA, Dar es Salaam

The post Gomes Ataja Dakika za Mabao Simba appeared first on Global Publishers.

Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment


 

Je Wajua??Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

Edusportstz